County Updates, Local Bulletins

WITO WATOLEWA KWA WAZAZI KAUNTI YA MARSABIT KUWA MFANO WA KUIGWA NA WATOTO WAO

NA Sebalua Moses

Ripoti ya wizara ya afya nchini imesema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana huku mmoja kati ya vijana 11 ni mraibu wa dawa za kulevya.

Ripoti hiyo pia imeorodhesha pombe, miraa  pamoja na sigara kama  dawa za kulevya ambazo hutumika zaidi mno.

Mwanahakarati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya katika kaunti ya Marsabit Fred Ochieng amesema kuwa matumizi ya dawa ya kulevya miongoni mwa vijana nchini iko juu zaidi.

Hata hivyo Ochieng ametoa wito kwa wazazi kushirikiana kwa pamoja ili kusaidia watoto wao sawa na kuwataka wazazi kuwa mfano mzuri ili watoto wasiige tabia zao

Wakati huo mwanaharakati huyo amesema ni sharti washirikiane kwa pamoja kwani ni  jukumu la kila mtu katika kaunti ya Marsabit kusaidia katika kupambana na kero hilo la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana

Subscribe to eNewsletter