County Updates, Local Bulletins

WITO WATOLEWA KWA WANANCHI WA MARSABIT KUJITOKEZA NA KUTAFUTA MSAADA WANAPOKABILIWA NA MATATIZO YA AFYA YA AKILI.

Na Caroline Waforo

Mtaalam wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Victor Karani amelalamika ongezeko la visa vya unajisi katika kaunti hii ya Marsabit huku akibaini kuwa visa hivyo hupelekea pia waathiriwa kukumbwa na matatizo ya afya ya akili.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani Karani amesema kuwa matatizo ya afya ya akili yanaambatanishwa na visa hivi.

Karani amekariri kuwa wengi wa wanaotekeleza visa hivi wanakabiliana na matatizo ya kiakili jambo linalofaa kushughulikiwa kwa dharura.

Vile vile mtaalam huyu wa afya ya akili ametoa wito wa watu kujitokeza na kutafuta msaada wanapokabiliwa na matatizo haya.

Kauli yake inajiri huku ulimwengu ukiadhimisha mwezi wa kuhamasishaji umaa kuhusiana na matatizo ya afya ya kiakili na kutilia mkazo katika umakini unaohitajika kwa umuhimu wa afya wa kiakili.

Subscribe to eNewsletter