Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Siku kama ya Leo miaka 19 iliyopita, Taifa liliwapoteza viongozi pamoja na wanaharakati waliokuwa kwenye ziara ya Amani kaunti ya Marsabit.
Biwi na simanzi lilitanda katika kaunti ya Marsabit amabayo kipindi hicho ikijulikana kama wilaya ya Marsabit, baada ya kuwapoteza viongozi mahiri ambao walikuwa na maono ya kuleta amani baina ya jamii zilizokuwa zinazozana.
Wabunge wote wanne waliokuwa wamechaguliwa kutoka maeneo bunge manne ya Moyale, North Horr Saku na Laisamis waliangamia katika ajali ya ndege iliyotokea siku hiyo katika eneo la Kofia Mbaya vyungani vya mji wa Marsabit.
Hata hivyo miaka 19 baadae angalau wananchi wa jimbo la Marsabit wana jambo la kujivunia ambalo ni Amani na uiano kati jamii zinazoishi hapa jimboni kama wanavyosema baadhi ya wananchi walizungumza nasi.
Wananchi pia wametoa wito wa Amani kudumishwa kikamilifu na kuhakikisha kwamba jimbo la Marsabit linasonga mbele kimaendeleo.
Wametoa wito kwa viongozi kuwa kwenye mstari wa mbele kuhubiri Amani na kuunganisha jamii ili kuhakikisha kwamba kaunti ya Marsabit hairudi katika machafuko yaliyoshuhudiwa awali.