Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Moses Sabalua,
Wito umetolewa kwa wasichana hapa jimboni Marsabit kujiunga na mashirika mbalimbali ya watawa na baadea kutumika kuendeleza ijili.
Akizungumza na idhaa hii mtawa kutoka shirika la Fransiscan Sisters of St Joseph, mtawa Monica Anastacia amesema kuwa shirika hilo lipo tayari kuwakaribisha wasichana wote ambao wangetaka kujiunga na shirika hilo ambalo tawi lake lipo katika Parokia ya Sololo.
Vilevile mtawa Monica amesema kuwa wasichana kujiunga na shirika hilo kutasaidia katika kuendeleza injili yake Kristo pamoja na kuwasaidia kukua kiroho.