Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng
Wazazi kutoka kaunti ya Marsabit wamekumbatia maamuzi ya mahakama kuu kufutilia mbali ulipaji wa karo kupitia mfumo wa E-Citizen.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha wazazi jimboni Marsabit Ali Noor amesema kuwa hatua ya Mahakama kukataa ulipaji wa karo kupitia E-Citizen ni afueni kwa wazazi katika maeneo kame ambao wanang`ang`ana kuwalipia wanao karo haswa ikizingatiwa kuwa eneo hili ni pana na kuna maeneo ambayo yana changamoto ya mtandao.
Akizungumza na idhaa hii, Noor ameipongeza hatua ya mahakama ya kutupilia mbali agizo hilo akitaja kuwa ni maamuzi mema na itawasaidia wazazi ambao wanategemea maafikiano baina ya walimu wakuu kuhusu mbinu za kulipa karo.
Ali amesema kuwa hali ya shule za mashinani katika kaunti ya Marsabit haingeweza kukumbatia malipo ya karo kupitia E-citizen huku akiitaka serekali kuweza kuangazia masuala haya wakati wanapofanyia mfumo wa elimu Marekebisho.
Na huku wanafunzi wakiwa nyumbani kwa likizo fupi ya mwezi wa nne, Ali amewarai wazazi kuwa karibu na wanao ili kuwafunza maadili mema.