KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Caroline Waforo na Isaac Waihenya
Huku ulimwengu ukiadhimisha mwezi wa kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa wa tawahudi yaani Autism wazazi katika kaunti ya Marsabit, wametakiwa kutowaficha watoto wanaougua ugonjwa huo.
Ni wito ambao umetolewa na mtaalam wa huduma kwa walemavu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Millicent Aoro ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani afisini mwake.
Kulingana na Aoro hili litawasaidia watoto hao kuishi maisha ya kawaida kwani wanapitia changamoto nyingi kutokana na ugonjwa huu kudhoofisha ukuaji, au ujuzi na uwezo wa mtoto wa kufikiria.
Vilevile ameitaka jamii kukomesha unyanyapaa dhidi ya watoto walio na ugonjwa wa tawahudi pamoja na kutupilia mbali dhana kuwa ugonjwa huo unatokana na laana.
Aoro anaeleza kuwa ugonjwa huu ambao hutatiza jinsi akili hufanya kazi una dalili mbalimbali zinazofungamana na kudhoofika kwa uwezo wa mahusiano ya kijamii, mawasiliano na hata mabadiliko ya tabia.
Dalili hizi hugunduliwa mtoto anavyoendelea kukua kama anavyoeleza Aoro.
Aoro ameweka wazi kuwa ugonjwa huu wa tawahudi hauna tiba ila madaktari huthibiti tu hali ya mwathiriwa.
Visa vya ugonjwa huu vinashuhudiwa hapa jimboni Marsabit huku wazazi wakitakiwa kuwapeleka wanao hospitalini ili ugonjwa huu kutambuliwa kwa mapema na kurahisisha mbinu za kuuthibiti pia kwa mapema.
Kuanzia mwezi juni mwaka 2024 hadi mwezi huu wa April 2025 visa 11 vya ugonjwa huu vimeripotiwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.