Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhakikisha kwamba wanoa ambao wametimiza umri wa kwenda shule wanajiunga na tasisi za elimu ili kupata elimu.
Kwa mujibu wa waziri wa elimu hapa jimboni Bi. Ambaro Abdullahi nikuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu ili kujifaidi katika maisha yake ya baadae.
Akizungumza na Idhaa hii ofisini mwake waziri Ambaro amesema kuwa watoto wote wa shule za chekekea jimboni Marsabit ambao ni 23,000 wamerejea shuleni kwa muhula wa pili baada ya shule kufunguliwa mapema wiki hii.
Aidha waziri Ambaro amesema kuwa serekali ya kaunti imeweka mikakati kabambe ya kuwapa watoto hao chakula wakiwa shuleni.
Vilevile Waziri Ambaro ametaja kwamba shule zote za chekechea zina walimu wanaohakikisha kwamba wanafunzi hao wanapata elimu bora.
Kuhusiana na swala ufadhili wa elimu haswa kwa wanafunzi wanaofadhiliwa na serekali ya kaunti ya Marsabit,waziri Ambaro amewataka wazazi wa wanafunzi wanaopata ufadhili huo kuwa na subira ili kuruhusu maswala yaliyomo mahakamani kuhusiana na ufadhili huo kukamilika.
Ambaro ametaja kwamba punde tu swala hilo litakapotatuliwa,basi serekali ya kaunti itaendeleza majukumu yake ya kulipa karo kwa wanafunzi wote.