Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Caroline Waforo,
Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa inabuni nafasi za ajira kwa vijana nchini ili kutatua nyingi za changamoto zinazoshuhudiwa miongoni mwao katika kaunti ya Marsabit na hata kitaifa.
Ni wito ambao umetolewa na mwanaharakati wa kutetea haki za kinadamu katika eneo la Loglogo Alice Leparie.
Leparie ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu amesema kuwa wakati mwingi vijana wanajihusisha na visa mbalimbali vya utovu wa kinidhamu ikiwemo utumizi ya dawa za kulevya kutokana na ukosefu wa ajira.
Na huku vijana walio chini ya umri wa miaka 18 wakitajwa kutumia pombe na dawa za kulevya jimboni Marsabit, Leparie ameitaka serikali pamoja na wadau mbalimbali jimboni kuweka mikakati ya kuwashirikisha wanafunzi kipindi hichi cha likizo ndefu ya mwezi Aprili ili kuwaepusha na visa kama hivyo.
Vile vile amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya wanao ili kuwakinga dhidi ya dhulma mbalimbali za kijinsia msimu wa likizo ikiweo visa vya unajisi na ubakaji.
Kadhalika Leparie amewataka wakaazi jimboni kuzidi kuwapa masomo wanao huku pia akiwatahadharisha dhidi ya kuwaoza wasichana wao mapema kwani ni ukiukaji wa haki za watoto kulingana na sheria.