County Updates, Local Bulletins

WAZAZI KAUNTI YA MARSABIT WAMETOLEWA RAI KUNYOSHA MIENENDO YA WATOTO WAKATI HUU WA LIKIZO.

Sheikh Mohamed Nur – Jamia Mosque Marsabit

Na Samuel Kosgei

Wazazi kaunti ya wametakiwa kuwa waangalifu dhidi ya mienendo na tabia ya watoto wao hasa wakati huu ambapo shule zimefungwa kwa likizo ya muhula ya kwanza.

Imam wa msikiti wa Jamia hapa mjini Marsabit Sheikh Mohammed Nur amewataka wanafunzi pia kusikiliza ushauri wa wazazi ili kuepuka majaribu na makundi ya kupotosha.

Ushauri sawa na huo umetolewa na mwanzilishi wa shirika la kutetea haki za wanawake kaunti ya Marsabit MWADO, Nuria Gollo ambaye amewarai wazazi kutoa ushauri nasaha kwa watoto wao ili wasipotoke kimaadili.

Nuria aidha ameonya wazazi dhidi ya kuwakeketa wasichana wadogo msimu huu wa likizo.

Subscribe to eNewsletter