Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng,
Serekali ya kaunti ya Marsabit kwa ushirikiano na serekali kuu pamoja na washikadau tofauti kupitia idara ya afya inatarajiwa kuzindua zoezi la chanjo ya polio wiki hii.
Kwa mujibu wa afisa wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Abdi Adan na ambaye ni meneja wa kituo cha kushughulikia maswala ya dharura katika kaunti ya Marsabit, ni kwamba chanjo ya polio hapa jimboni imechochewa na mlipuko wa wa ugonjwa wa polio nchini Ethiopia ambao umelazimu serekali kuchukuwa hatua za dharura ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo nchini.
Adan amesema kuwa kupitia ushirikiano na serekali kuu, shirika la afya ulimwenguni (WHO), pamoja na UNICEF na AMREF, idara hiyo itahakikisha kwamba chanjo hii imeweza kusambazwa katika zahanati na hospitali zote jimboni huku zoezi hili likitarajiwa kung`oa nanga tarehe 11 mwezi huu wa nne.
Aidha Adan ameelezea kuwa zoezi hili linalenga watoto walio chini ya umri wa miaka 11 ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Hata hivyo Adan amewarai wakazi wa Marsabit kuweza kukumbatia chanjo ya polio ili kusaidia katika kuboresha afya ya jamii.
Kuhusiana na mripuko wa ugonjwa wa Surua maarufu Measles katika eneo la Moite Adan afisa huyu wa afya ameelezea kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit inashirikiana na washikadau katika kuendeleza chanjo dhidi ya ugonjwa huo uliripotiwa majuma machache yaliyopita katika wadi ya Loiyangalani hapa jimboni Marsabit