County Updates, Local Bulletins

WATOTO 3,448 KATIKA ENEO LA MOITE, WADI YA LOIYANGALANI WAPEWA CHANJO YA UNGONJWA WA SURUA.

Na Isaac Waihenya,

Idara ya afya kaunti ya Marsabit imewapa chanjo ya ugonjwa wa Surua maarufu (Measles) watoto 3,448 katika eneo la Moite, wadi ya Loiyangalani.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa afya katika kaunti ndogo ya Laisamis Yussuf Galmogle ni kuwa idadi hiyo imeafikiwa kutokana na ushirikiano kati ya wahudumu wa afya kauti ya Marsabit pamoja na madaktari wasio ni mipaka nchini MSF.

Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Galmogle ameweka wazi kuwa zoezi la utoaji chanjo linaendelea huku wakilenga takriban watoto 3,907 katika eneo la Moite pekee.

Aidha afisa huyu wa afya ametaja kwamba zoezi hilo limetatizwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika eneo hilo kwa muda wa wiki mbili sasa.

Subscribe to eNewsletter