Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Samuel Kosgei
ASKOFU wa kanisa la Kiaglikana (ACK) jimbo la Marsabit Daniel Wario Qampicha amesisitiza haja ya washikadau wote kaunti ya Marsabit kushirikiana pamoja na kusaidia katika jitihada za kuwaondoa wakimbizi wa machafuko ya kikabila walio katika eneobunge la Saku.
Akizungumza hii leo kwenye mkao wa kujadili suluhu ya kusaka Amani ya kudumu kaunti ya Marsabit Askofu Qampicha alisema kuwa itakuwa vigumu kama jimbo kusonga bila kusuluhisha kero la uwepo wa wakimbizi.
Ameitaka mashirika ya kibinafsi, serikali zote mbili n ahata wananchi wenye nia njema kuwapa msaada wakimbizi wa vita ili kupata makao mema.
Sheikh Bashir Somo kwa upande wake amekariri haja ya wananchi kumuogopa Mungu na kufuata mafunzo ya dini yanayopinga vikali dhulma na mauaji ya binadamu. Amewataka pia wakuu wa usalama kuzidi kuhusisha viongozi wa kidini katika mikakati ya kusaka Amani ya kudumu.
Naibu Mwenyekiti wa kamati ya Amani jimbo la Marsabit Adan Chukulisa amependekeza jamii kuhusisha wazee, vijana na akina mama katika kufanya maamuzi ya kusaka Amani kwenye jamii.
Ametaka viongozi wa kisiasa kukoma kuchochea jamii zao kwenye masuala ya kisiasa.
Ugavi sawa wa nafasi za ajira za jimbo pia imetajwa kuwa njia moja ya kuleta uwiano na utulivu miongoni mwa jamii.
Kikao hicho cha kujadili suluhu ya kudumu ya Amani Marsabit kilifanikishwa shirika la kanisa la kianglikana linalotoa huduma ya maendeleo kwa jamii Anglican Development Services ADS.