County Updates, Local Bulletins

WANAWAKE KAUTI YA MARSABIT WATAKIWA KUCHUKUA MIKOPO NA KUAZISHA AU KUIMARISHA BIASHARA ZAO.

Na JB Nateleng,

Wajane na akinamama wanaolea wanaao pekee yao wanafaa kuwa wabunifu kwa masuala ya kibiashara ili kustawisha familia na jamii kwa ujumla

Haya ni kwa mujibu wa Betty Musindai ambaye ni rais wa shirika la Hope of Life International.

Musindai ameelezea kwamba wajane wanafaa kuwa makini kwa masuala ya kibiashara na kuhakikisha kuwa wamejikaza kwa kuchukua mikopo ili waweze kujiimarisha na kujiinua kibiashara.

Kadhalika amewachangamoto wajane kuhudhuria hafla za kutoa hamasa kuhusu biashara ili wapate ujuzi wa kupanua na kusimamia biashara zao.

Na huku ulimwengu ukiadhimisha mwezi wa kutoa hamasa kuhusu afya ya akili, Musindai ameitaka serakali na mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kuangazia wajane kwani wanapitia changamoto nyingi ambazo zinadhuru afya yao ya akili.

Kiongozi huyu amewapa moyo wajane na akina mama wanaowalea wanao pekee yao kuwa wachangamvu na kujikaza ili kukimu mahitaji ya familia.

 

Subscribe to eNewsletter