County Updates, Local Bulletins

WANAONUFAIKA NA MPANGO WA INUA JAMII,MARSABIT WATAKIWA KUWA NA SUBIRA SEREKALI INAPOLAINISHA MIKAKATI YOTE KATIKA MPANGO HUO.

Picha Hisani

Na Isaac Waihenya,

Wanaonufaika na mpango wa kuwapa fedha zinazolenga kuinua maisha ya maskini,walemavu, pamoja na mayatima wa Inua Jamii katika kaunti ya Marsabit, wametakiwa kuwa na subira wakati serekali inapolainisha mikakati yote katika mpango huo.

Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kauti ya Marsabit Mukanzi Leakey ni kuwa serekali imejiza titi kuhakikisha kwamba wanaonufaika na mradi huo wanapokea fedha zao bila hitilafu zozote.

Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani ofisini mwake,Mukanzi amekiri kuwa japo kuna changamoto chache katika mradi huo ila serekali kupitia idari ya huduma za jamii imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba wanaonufaika wanapata fedha hizo kwa wakati na pia zinawafikia walengwa.

Mukanzi amewataka wanaokumbana na changamoto zozote kuhusiana na mradi huo kutembelea ofisi husika ili kupata usaidizi.

 

Subscribe to eNewsletter