County Updates, Local Bulletins

WANANCHI WATAKIWA KUTOA RIPOTI KUHUSU MASWALA YANAYOWEZA KUVURUGA AMANI JIMBONI MARSABIT.

Na Isaac Waihenya,

Naibu mwenyeki wa kamati ya amani katika kaunti ya Marsabit Adan Chukulisa amesifia hatua zilizopigwa katika kuimarisha Amani, kaunti ya Marsabit.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Chukulisa amelitaja swala la utovu wa usalama lililoshuhudiwa majuma machache yaliyopita katika eneo la Dukana kuwa limetatuliwa kikamilifu.

Chukulisa amekariri kuwa usalama umeimarishwa katika eneo hilo huku kamati ya amani ikiundwa kushughulikia maswala yanayoweza kujiri na kutatiza amani.

Aidha Chukulisa amekariri haja ya kudumisha uano kati ya jamii mbalimbali zinazoishi jimboni Marsabit ili kuhakikisha kwamba maendeleo yanasheni.

Vilevile naibu mwenyeki huyu wa kamati ya Amani, amewataka wananchi kutokubali kugonganishwa na wanasiasa huku akiwaonya wale wanolenga kuwagawanya wananchi kwa misingi ya kikabila.

 

Subscribe to eNewsletter