County Updates, Local Bulletins

WANANCHI MJINI MARSABIT WATOA HISIA ZAO KUHUSU ONGEZEKO LA DENI LA TAIFA.

Picha Hisani

Na Moses Sabalua,

Kufuatia ongezeko la deni humu nchini wananchi katika kaunti ya Marsabit wametoa hisia mseto kuhusiana na swala hilo ambalo wanahisi kuwa linaadhiri ustawi wa taifa.

Kauli zao zinajiri baada ya Rais William Ruto kuzuru taifa la China na kuweka mikakati ya kuendeleza miradi ya maendelo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka eneo la Naivasha hadi Malaba pamoja miradi mengine ya barabara.

Wakizungumza na idhaa hii baadhi ya wakaazi kutoka mjini Marsabit wamehoji kuwa deni la shilingi trillioni 11 ambalo Kenya inadaiwa hunda likaongezeka na kuadhiri Uchumi.

Hata hivyo baadhi yao wameelezea kuwa ukopaji wa pesa humu nchini hautasadia kwa sababu ya uwepo wa ufisadi.

Wakati uo huo baadhi yao wamemalamikia ongezeko la gharama ya maisha huku wakisema kuwa Wakenya wanaafaa kuwa waangalifu wanapowachagua viongozi wao.

Subscribe to eNewsletter