KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Joseph Muchai
Wafanyibiashara katika mji wa Marsabit wametoa hisia mseto kufuatia kushuka kwa bei ya mafuta na bidhaa za petroli. Wakiongea na shajara ya radio jangwani wengi wao wanaojihusisha na biashara ya uchukuzi wameshabikia hatua hiyo ya serikali wakiipongeza.
Hata hivyo wengine wanahisi kuwa wao kushukisha bei ya usafiri na bidhaa sokoni sawia na dukani halitawezekana kwani bei ya petroli imeshuka kwa kiwango kidogo mno.
Wakati uo huo wengine wametoa wito kwa serikali kushukisha bei ya petrol zaidi kwani gharama ya maisha ingali ipo juu. Wanahoji kuwa iwapo bei hiyo itaendelea kupungua gharama ya maisha itapungua kwa kiwango kikubwa.