Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng
Walimu wametakiwa kuwa na subira kuhusiana na suala la bima ya Afya huku tume ya kuajiri walimu TSC ikishirikisha washikadau kutoka Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) ili kutatua utata uliopo.
Kulingana na katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KUPPET tawi la Masabit Sarr Galgalo ni kwamba tume ya Kuajiri walimu TSC inashughulikia suala hilo huku akiwarai walimu kuweza kutembelea hospitali ili kupata huduma ya afya panapohitajika kwa sababu makato ya hapo awali ya NHIF yamehamishwa kwa SHA
Sarr ameelezea kwamba mvutano huu umesababishwa na mamlaka ya afya ya Jamii SHA kuitisha fedha nyingi kuliko ya bima ya Minet ambayo ilikuwa ikifadhili matibabu ya walimu.
Sarr ameitaka TSC kuzungumza na mratibu wa Bajeti ili kuharakisha mchakato wa kuwahamisha bima ya afya ya walimu kutoka Minet mpaka SHA.