County Updates, Local Bulletins

WALIMU KAUNTI YA MARSABIT WAPEWA MAFUNZO YA KIDIJITALI KWA LENGO LA KUPIGA JEKI MTAALA MPYA WA ELIMU (CBE).

Na Isaac Waihenya,

Warsha ya siku mbili ya kuwapa mafunzo ya kidijitali walimu wa shule za msingi na msingi sekondari (JSS) katika kaunti ya Marsabit imeongoa nanga hii leo.

Warsha hii inayofadhiliwa na shirika la Raspberry Pi Foundation na kutekelezwa na Baraza la maendleo la kaunti zilizopo maeneo kame (FCDC) inalenga kuwapa mafunzo ya kidijidali walimu 15 kutoka shule 12 za maeneo bunge yote manne ya kaunti ya Marsabit kama njia moja wapo ya kupiga jeki mtaala mpya wa elimu (CBE).

Akuzungumza wakti wa kufungua warsha hiyo Waziri wa elimu katika kaunti ya Marsabit Bi. Ambaro Abdullahi amepongeza hatua ya kuongezea maeneo bunge mawili ya North Horr na Moyale ambayo yalikuwa yameachwa nyuma huku akiweka wazi kuwa hilo litahakikisha kwamba maarifa ya teknolojia yanafika kila pembe ya jimbo hilo.

Aidha Waziri Ambaro ameyarai mashirika ya kijamii jimboni kushirikiana ili kuboresha kiwango cha elimu jimboni huku akiwataka walimu waliopata mafunzo hayo kuyatumia kuwaimarisha wanafunzi kidijitali.

Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri amepongeza hatua hiyo huku akitoa wito kwa shirika la Raspberry Pi Foundation na Baraza la maendeleo la kaunti zilizopo maeneo kame (FCDC) kuongeza idadi ya shule zinazonufaika na mpango huo.

Aidha mkurugenzi huyo ametetea mtaala mpya wa CBE kuwa una manufaa zaidi kwa wanafunzi ikizingatiwa kuwa wafikapo gredi ya tisa, wanapata fursa ya kuamua mwelekeo wao wa kitaaluma na hivyo kujibidisha zaidi katika mwelekeo huo.

Mradi huu unatekelezwa katika kaunti 10 kaunti zilizopo maeneo kame (FCDC) ambazo ni Marsabit Turkana, West Pokot, Lamu, Wajir, Isiolo, Tana River, Samburu, Garissa, na Mandera.

Subscribe to eNewsletter