KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, amethibitisha kuwa wakimbizi wa Kenya 4,993 walioko katika miji ya Dillo na Megado nchini Ethiopia wameonyesha nia ya kurejea nyumbani.
Dillo na Megado ni makazi ya wakimbizi katika eneo pana la jamii ya Oromia, Ethiopia, ambako wanahifadhiwa wakimbizi wa Kenya waliokimbia nchi yao kutokana na mapigano ya kikabila yaliyoanza mwaka 2000 na kusababisha mauaji ya Turbi mnamo 2005.
Makazi hayo ya wakimbizi yanakabiliwa na changamoto sugu, hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, kutokana na maeneo yao ya mbali na miundombinu duni, hali inayofanya iwe vigumu kwa mashirika ya misaada kutoa usaidizi ipasavyo.
Akizungumza na bunge la seneti Mudavadi alisisitiza kuwa ingawa serikali itasaidia katika kuwarejesha na kuwaunganisha tena na jamii zao, hakuna fidia yoyote itakayotolewa.
Kuna wanaume 2,788, wanawake 2,883, na watoto 3,385 katika kambi hizo za wakimbizi.
Seneta wa Marsabit, Mohamed Chute, alikosoa majibu ya Mudavadi, akisema hayakuridhisha na hayakuwa na muda maalum wa utekelezaji wa urejeshaji huo wa wakimbizi.