County Updates, Local Bulletins

Wakimbizi wa ndani kwa ndani walioathirika na machafuko ya kikabila mwaka wa 2022 katika kaunti ya Marsabit wapokezwa bidhaa za ujenzi.

Na Joseph Muchai,

Wahanga wa machafuko ya kikabila ya mwaka 2022 katika kaunti ya Marsabit wamepokea msaada wa bidhaa za ujenzi leo kwa hisani ya Kanisa la Kiangilikana.

Ni familia 25 ambazo zimenufaika kutokana na msaada huo ambao unajumuisha viuma misurmari pamoja mbao.

Akihutubu baada ya kutoa vifaa hivyo Askofu wa kanisa la Kiangilikana Daosisi ya Marsabit Askofu Daniel Qampicha amesema kuwa msaada huo unandamana na huduma za fundi ambazo pia ni kwa hisani ya kanisa hilo.

Wakati uo huo Askofu Qampicha ametoa wito wa ushirikiano miongoni mwa viongozi ili kuhakikisha kuwa wakaazi wanapata kurejelea maisha yao ya kawaida makwao.

Kwa upande wake Chifu wa eneo la Sagante Jaldesa Abdul Hussein amesema kuwa msaada huo utawafaa zaidi wananchi huku akiwataka kuruhusu mafundi watakaotumwa kufanya ujenzi kwani malipo yao yatagharamiwa na wahisani.

Kwa upande wao wakimbizi hao wameonesha furaha yao wakiutaja msaada huo kama mwanzo mpya kwani kwa muda wa miaka mitatu sasa wamekuwa wakihangaika bila makao.

Subscribe to eNewsletter