KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Imebainika kuwa wakenya wanakopa zaidi ya shilingi millioni 500 kwa siku na shilingi billioni 15 kwa mwezi kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la Digital Financial services Association of Kenya (DFSAK).
Mtaalam wa masuala ya kifedha katika kaunti ya Marsabit John Maina katika amesema kuwa ongezeko hilo la kuchukua mikopo ya digitali imechangiwa na kuongezeka kwa gharama ya maisha pamoja na kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi haswa walioajiriwa kwenye mashirika ya kibinafsi na serikali za kaunti .
Kulingana na Maina Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya wakenya millioni 8 wanatumia njia ya digitali kuchukua mikopo hiyo..
Aidha John amesema kuwa mikopo hiyo ya digitali imewafanya wakenya kutowekeza katika akiba zao hiyo kufanya maisha kuwa magumu zaidi.