County Updates, Local Bulletins

WAKAZI WA ENEO LA SHAURI YAKO MJINI MARSABIT WAMESEMA KUWA BARABARA ZA MAENEO HAYO ZINAHATARISHA MAISHA YA WASAFIRI WA MIGUU

Shauri Yako – Marsabit Town

Na Samuel Kosgei

WAKAZI wa eneo la Shauri Yako mjini Marsabit na sehemu za karibu wamesema kuwa kwa muda sasa barabara za maeneo  hayo zinahatarisha maisha ya wasafiri wa miguu kutokana na kukosekana kwa sehemu ya watu wa miguu kupitia.

Wakizungumza na shajara wakaazi hao haswa – wanabodaboda na wafanyibiashara wamesema kuwa kutokana na wembamba wa barabara hiyo – watu, magari na bodaboda zinang’ang’ania barabara hiyo suala wanalosema linahatarisha maisha ya wanatembea kwa miguu.

Kwa kawaida ni watu ndio huondokea magari barabarani lakini mjini Marsabit na viunga vyake ni magari ndio huondokea wanaotembea kwa miguu.

 

Subscribe to eNewsletter