County Updates, Local Bulletins

WAKAZI ILLERET MARSABIT WAITAKA IDARA YA AFYA JIMBONI MARSABIT KUWANUNULIA AMBULENSI ILI KUWANUSURU WAKATI WA DHARUARA.

Illeret, Marsabit County

Na Samuel Kosgei

WAKAZI eneo la Illeret eneobunge la North Horr wameendelea kutoa ombi kwa idara ya afya jimboni Marsabit kuwanunulia gari la kubeba wagonjwa wa dharura  yaani ambulensi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo.

Wakizungumza katika eneo hilo wakaazi hao wakiongozwa na fauzia silamo wamesema kuwa akina mama mara nyingi huteseka sana wanapokaribia kujifungua kutokana na ukosefu wa gari la ambulensia suala wanalosema limechangia kupotea kwa maisha ya akina mama au mtoto.

Sasa wanaitaka serikali ya jimbo kupitia idara ya afya kuwakumbuka kwenye suala hilo linalohusu afya.

Wakaazi hao pia wameirai serikali yake gavana Mohamud Ali kuwachimbia visima vya maji karibu nao ili kuepushia akina mama mateso ya kwenda kusaka maji ya matumizi sehemu za mbali.

Rose Loshere mkaazi wa eneo hilo anasema kuwa magonjwa yanayosababishwa ba maji machafu yanashuhudiwa sana katika eneo hilo hivyo kurai vingozi wao kutowasahau na kuwahudumia kama wakenya wengine.

Aliongeza kuwa akina mama wajawazito huhangaika kwenda sehemu za mbali kusaka maji ya matumizi manyumbani.

Subscribe to eNewsletter