Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Muchai Joseph
Wakaazi wa Marsabit wametoa maoni yao mseto kuhusiana na azma ya aliyekuwa waziri wa elimu Fred Matiang’i kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongea na Shajara ya Radio Jangwani baadhi ya wakaazi hao wameonesha matumaini yao kuwa Matiang’i ana uwezo wa kubadilisha mfumo wa uongozi kama alivyofanya kwenye wizara ya elimu.
Hata hivyo wengine wao wanahisi kuwa Matiangi hawezi kuwa kiongozi wa nchi wakisema kuwa haiwezekani kulinganisha uratibu wa wizara na usimamizi wa nchi nzima.
Haya yanajiri huku Daktari Fred Matiang’i akifanyiwa Zaira ya makaribisho ya hadhara katika kaunti ya Kisii hii leo.