KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Moses Sabalua,
Afisa mkuu anayesimamia idara ya kutoa na kuhifadhi damu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Diba Molu, amesisistiza haja ya wananchi kujitolea mara kwa mara kutoa damu ili kuokoa maisha hapa jimboni.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Diba amesema kuwa idara hiyo hushuhudia ukosefu wa damu kwani mahitaji yake ni mengi kuliko idadi ya wanajitolea kutoa damu.
Aidha Diba amesema kuwa idara hiyo inakosa kupata damu kufikia kiwango kinachohitajika ambacho ni ‘Pinti’ mia tatu kwa mwezi.
Wakati uo huo Diba amewataka wakaazi wa Marsabit kuwa mstari wa mbele kusaidia katika kutoa damu kwani ina manufaa zaidi huku akisema kuwa idara hiyo imeimarisha huduma za kutunza damu ili kusaidia wagonjwa pindi tu itakapohitajika.