Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kukumbatia mbinu mpya ya kupokea fedha zinazolenga kuinua maisha ya maskini,walemavu, pamoja na mayatima za Inua Jamii.
Kwa mujibu wa mkurugenzi katika idara ya hudumu ya jamii katika kaunti ya Marsabit Vincent Musee ni kuwa baadhi ya changamoto ambazo wananchi wanalalamikia zinaweza tatulika iwapo tu wananchi watakuwa waaminifu na waukumbatie mpango huo mpya wa serekali.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Musee amesema kuwa moja wepo ya changamoto ambazo zinakumba mbinu hiyo mpya ni ikiwepo wanaowasaidia wazee kutaka kuandikisha namba zao ili kupokea fedha jambo ambalo serekali imelipiga marufuku.
Ha hivyo Musee amekanusha madai kuwa henda fedha za wanaofaidika na mradi huo zikarejeshwa kwa idara iwapo watakawia kuzitoa kwa simu kwa ajili ya matumizi.