Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Samuel Kosgei
Baadhi ya wakaazi wa Marsabit wamepinga mapendekezo ya seneta wa kaunti ya Marsabit Moses Kajwang aliyependekeza kaunti nchini zipunguzwe hadi 13 kutokana mzigo ambao taifa haliwezi kulibeba.
Wananchi waliosema nasi kwenye kipndi cha Amkia Jangwani hii leo wamesema kuwa kupunguza kaunti itamaanisha kuwa huduma kwa mwananchi aliye mashinani itapatikana mbali ikilinganishwa na sasa.
Hata hivyo wanasema licha ya kutaka kaunti kusalia ilivyo wangependa magavana kote nchini haswa Marsabit kuwajibika na kuwahudumia wakenya bila ubaguzi.
Wakati uo huo wengineo wameunga mkono mapendekezo hayo wakidai kuwa wizi wa mali ya umma umekolea katika serikali za kaunti na hivyo kuna haja ya kudhibitiwa mara moja. Wanadai kuwa licha kaunti kuwa nyingi bado huduma hazifikii mwananchi.