Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Muchai Joseph
Huku wakenya wakiadhimisha sikuku ya Leba dei hii leo wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametoa maoni yao kuhusu siku yenyewe.
Wakiongea na Shajara Ya Radio Jangwai baadhi ya wakaazi ambao wengi ni wafanyibiashara wameelezea sababu ya kutokusherehekea siku hii kama miaka ya hapo awali wakitaja kwamba hilo linachochewa na hali ngumu ya uchumi.
Aidha wakaazi hao wameelezea kuwa kupanda kwa gharama ya maisha kumechangia katika kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu hivyo basi kulemewa kuenda mapunzikoni wakati wa sikukuu ya wafanyikazi.
Hata hivyo wengi wao wanahoji kuwa uporaji wa mali ya umma na kutokuwajibika kwa viongozi wa kisiasa kumesababisha wakenya kukosa sababu ya kufurahia mchango waokatika ujenzi wa taifa.
Kwa kawaida siku hii huwa ya kusherekea mchango wa wafanyi kazi katika ukuaji wa uchumi kote duniani.