KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Joseph Muchai
Wakaazi wa Marsabit wamelalamikia jinsi hali ya maisha yanavyoendelea kuwa magumu yakilingashwa na miaka ya hapo awali hivyo kushuka kwa viwango vya furaha.
Wengi walioongea na kituo hiki wanasema kuwa hali ya sasa imechangiwa na gharama ya juu ya bidhaa kutokana na mabadiliko katika mfumo wa uongozi.
Aidha baadhi wanasema kuwa gharama ya juu imesababishwa na ongezeko katika mishahara ya wawakilishi hususan katika nyadhifa za uongozi.
Hata hivyo kwa upande wake Charles Maina ambaye ni mfanyi biashara mjini Marsabit amesema kuwa maisha hajabadidlika na kukariri kuwa furaha hutegemea mtu binafsi. Pia nasema kuwa ni kutokana na mashaka wanayojisababishia wenyewe ambapo wengi wanaishia kuwa na msongo wa mawazo. Sasa anashauri watu kuishi kulingana na kipato pasipo kujitia mawazo.
Haya yanajiri muda mfupi tuu baada ya utafiti kuonyesha kuwa sita kati ya wakenya kumi wana furaha maishani. Miongoni mwa mambo yaliyotajwa kuchangia katika furaha ya miongoni mwa watu ni elimu, hali ya kifedha, idadi ya marafiki, hali ya ndoa, afya, tabia ya mtu binafsi miongoni mwa maswala mengine.
Kulingana na utafiti huo watu wenye furaha Zaidi ni walio kati ya umri wa miaka 30 na 34.