County Updates, Local Bulletins

WAKAAZI WA LEYAI SAKU, MARSABIT WALALAMIKIA ZAHANATI ILIYOJENGWA MIAKA 9 ILIYOPITA ILA HAITUMIKI.

Leyai Displaced Dispensary

Na Mwandishi Wetu

WAKAAZI wa Leyai, wadi ya Karare kaunti ya Marsabit wameonesha masikitiko makubwa kutokana na kukosa huduma za hospitali karibu nao.

Wakaazi hao wa Leyai wamekosoa pakubwa serikali ya Marsabit kupitia idara ya afya kutokana na kusahaulika na kupuuzwa kwa  zahanati ya Leyai iliyojengwa mwaka wa 2016.

Wananchi wanasema kuwa wanapitia mahangaiko makubwa kusaka matibabu sehemu za mbali kama vile Songa au mjini Marsabit licha ya zahanati kujegwa hapo miaka tisa iliyopita ila imechakaa kutokanana na kutofunguliwa rasmi. Akina mama wajawazito na watoto wanatajwa kuhangaika sana wanaposaka matibabu.

Kulingana na wakazi hao watu wanaowasaidia kwa sasa ni wahudumu wa afya wa kujitolea CHPs ambao mara kwa mara ndio wanaoonekana wakitoa huduma ya kwanza na jamii japo.

Suala linguine kero kwao ni ubovu wa barabara wanayosema kuwa inarejesha nyuma huduma za kusafirisha wagonjwa wakati wa dharura.

Kauli yake mama huyo imesisitizwa na mwanaharakati wa haki za kibinadamu Mohamed Hassan ambaye anasema haki ya kimsingi za kupata matibabu kwa wakaazi wa Leyai zimekiukwa na serikali ya jimbo ambayo ndio inasimamia huduma za matibabu.

Mohamed ametolea wito serikali ya kaunti kupitia idara ya afya kurekebisha zahanati hiyo na kufunguliwa rasmi ili iwe yenye manufaa kwa wananchi wa Leyai. Anasema kuwa rasilmali ya serikali ilitumika kujenga zahanati hiyo, hivyo kuna haja ya kurekebishwa na kuhudumia wakaazi.

Subscribe to eNewsletter