Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Henry Khoyan,
Huku maeneo mbalimbali jimboni Marsabit yakiendelea kushuhudia mvua, wakaazi wa eneo la Karare wametolewa wito wa kuwa wangalifu na kujali usalama wa wanao.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kupitia njia ya simu,chifu wa eneo la Karare Magdaline Ilimo amewarai wazazi kuhakikisha kwamba wanajali maslahi na wanao na kutowapa majukumu ambayo yanaweza hatarisha maisha yao.
Kauli ya chifu Ilimo inajiri kufuatia kisa ambapo mtoto mmoja wa umri wa miaka 6 alipoteza maisha baada ya kutumbukia kwenye tenki la maji mnamo siku ya jumamosi tarehe 3 mwezi huu wa Mei.
Aidha chifu Ilimo amewataka wazazi kufunika tenki za maji na pia kuwa wangalifu Zaidi ili kuzuia Mikasa kama hiyo ambayo inaweza epukika.
Mwili wa marehemu ulizikwa katika eneo hilo la Karare.