Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
NA Isaac Waihenya
Wakaazi wa eneo la Mado Adi katika lokesheni ya Waiye, eneo bunge la Moyale kauti ya Marsabit, wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kusaulika na serekali ya kaunti ya Marsabit.
Wakizumgumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, wakaazi hao wakiongozwa na mzee wa kijiji Wako Liban Halakhe wametaja kwamba kwa muda wa miezi mitano sasa barabara ya kutoka eneo hilo kuelekea Sololo mjini haijakuwa ikipitika kutokana na mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kuikarabati kuchimba mtaro mkubwa na kisha kuuwacha vile.
Wakaazi hao wanalalama kuwa hilo limepelekea Barabara hiyo kutopikika na kuwazuia kupata huduma muhimu kama vile huduma za afya ambazo huwa wanasaka katika eneo la Sololo pekee.
Wametaja kuwa licha ya kuwasilisha lalama zao kwa gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamed Ali na hata baadae kumtuma waziri wa maji na mazingira Bi. Grace Galmo kutadhimini hali bado hakuna hatua zozote zimechukulia miezi mitano baadae.
Wameitaka serekali ya kaunti kufanya hima na kuwaondolea kero hilo ambalo wanataja kwamba linaadhiri maisha yao ya kimsingi.
Kando na hilo wakaazi hao wamelalamikia kero la ukosefu wa maji, kwani kisima pekee kilichopo eneo hilo hakina maji huku wakiitaka serekali kughughilika kero hilo haraka iwezekanavyo.