County Updates, Local Bulletins

WAKAAZI WA ENEO LA DUKANA WATAHADHARISHWA DHIDI YA KUENEZA PROPAGANDA ZINAZOWEZA KUCHANGIA KATIKA KUVURUGA AMANI.

County Commissioner Marsabit

Na Mwandishi Wetu,

Wakaazi wa maeneo ya Dukana kaunti ya Marsabit na wale Dillo nchini Ethiopia wametahadharishwa dhidi ya kueneza propaganda zinazoweza kuchangia katika kuvuruga amani inayoendelea kusheheni katika maeneo hayo majuma kadhaa baada ya matukio ya utovu wa usalama kushuhudiwa.

Kulingana na kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau wakaazi wa maeneo hayo ya mpakani wametakiwa kuishi kwa umoja na pia kuhakikisha kuwa wanaripoti visa vyovyote vya utovu wa usalama kwa idara ya usalama.

Kamishna Kamau aliyasema haya baada wa mkutano wa amani uliofanyika tarehe 2 mwezi huu wa Aprili katika eneo la Dillo nchini Ethiopia ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Dillo Jillo Dida pamoja na naibu kamisha wa kaunti ndogo ya Dukana Charo Katana.

Katika mkutano huo kamati ya amani pia iliweza kuundwa ikijumuisha wanachama 35 kutoka eneo la Dukana sawa na maeneo yaTaltale and Dilo nchini Ethiopia.

Mikakati hiyo iliafikiwa huku maafisa wa jeshi la ulinzi KDF wakiendeleza operesheni ya ‘Ondoa Jangili’ katika eneo la Dukana ili kuwaondoa wahalifu wa kundi la OLF wanaoaminika kuendeleza shughuli zao katika eneo hilo.

Subscribe to eNewsletter