Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Sabalua Moses,
Kufuatia mdahalo kuhusu hazina ya maendeleo ya maeneo bunge nchini NGCDF kuondolowa kutoka kwa wabunge na badala yake kutolewa na serekali kuu, wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametoa hisia mbalimbali kuhusiana na swala hilo.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani,wametaja kwamba pendekezo hilo litawafaa sana haswa ikizingatiwa kwamba baadhi ya walengwa katika jimbo hili hukosa kunufaika na mgao huo kutokana na kuutengwa kwa misingi ya kikabila.
Wakati uo huo baadhi yao wamesema kuwa fedha hizo zimekuwa zikiwasaidia wananchi kwani wengi wa Wakenya wanaweza kuwafikia wabunge kwa urahisi.
Hata hivyo wengine wao wameelezea kufaidika na pesa hizo za CDF wakisema kuwa kwa miaka mengi fedha hizo zimeweza kufadhili masomo hapa jimboni huku wakipendekeza zienadelee kutolewa kupitia ofisi za maeneo bunge na sio serikali kuu.