County Updates, Local Bulletins

WAKAAZI MARSABIT WATOA HISIA MSETO KUHUSIANA NA UPINZANI KUTAKA KUHUSISHWA KWENYE ZOEZI LA KUTEUA MAKAMISHNA WA IEBC

Na Henry Khoyan

Wakaazi jimboni Marsabit wametoa hisia mseto kuhusu swala la upinzani kuhusishwa katika mchakato wa kuteua mwenyekiti na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Wametaja kwamba ni muhimu upinzani ihusishwe ili kuhakikisha uwazi na usawa katika mchakato huo.

Hata hivyo Kauli yao imepingwa na Benard Bonaya ambaye kulingana naye rais ana mamlaka na anafaa kuteua makamishna hao bila ya kuhusishwa upinzani kwani haipo kwenye sheria za taifa hili.

Subscribe to eNewsletter