County Updates, Local Bulletins

WAKAAZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI MSIMU HUU WA MVUA

Na Joseph Muchai

Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwa waangalifu ili kuepukana na maafa yanayotokana na mvua kubwa.

Akiongea na kituo hiki kamanda wa polisi wa Marsabit Leonald Kimaiyo amewataka walio kwenye nyanda za chini kutafuta usalama kwenye nyanda za juu sawa na walio kwenye mikondo ya maji almaarufu laga kuhamika maeneo salama.

Aidha walio kwenye maeneo yenye historia ya kufurika maji msimu wa mvua wametakiwa kuwa waangalifu Zaidi. Loyangalani na North Horr ni baadhi ya maeneo yanayotajwa kushuhudia mafuriko msimu wa mvua.

Haya yanajiri huku hali ya mvua ikiendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti hii na nchi kwa ujumla.

Itakumbukwa kuwa wiki jana baadhi ya wafanyibiashara maeneo ya Old Town mjini Marsabit walikadiria hasara baada ya mvua ya usiku kucha kusababisha mafuriko yalioingia kwenye maeneo yao ya biashara na kusababisha kuharibika kwa bidhaa za biashara.

Subscribe to eNewsletter