County Updates, Local Bulletins

WAKAAZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMELEEZA HISIA KUHUSIANA NA RIPOTI YA KAMARI INAYOORODHESHA WALIMU KUWA MSARI WA MBELE KUCHEZA KAMARI

Marsabit Town

Na Sebalua Moses

Kufuatia ripoti iliyotolewa hivi maajuzi  walimu wamekuwa mstari wa mbele katika orodha ya wachezaji Kamari humu nchini na kuwapiku  askari,madereva,waendeshaji bodaboda na  wauzaji mboga.

Hata hivyo wakaazi katika kaunti ya Marsabit wameleeza hisia mseto kuhusiana na ripoti hiyo wengi wakieelezea kuwa wengi wa walimu hupokea mishahara kila mwezi hivyo kuwapa nafasi katika kushiriki katika Kamari.

Vile vile baadhi yao wameeleza kuwa walimu  pamoja na askari ni mashabiki wa soka hivyo kupelekea wengi wao kuvutiwa na mchezo wa Kamari ili kupata faida wanapotazama michuano hiyo.

Kwa upande wake Collins Wese mmoja wa wakaazi ameeleza kuwa Askari  nao hujihusisha na Kamari wakati ambapo wapo kazini  kwani huwa na wakati mwingi wa kukaaa hiyo basi hujipata kuhusika katika mchezo wa Kamari ili kutafuta jambo la kufanya.

Kulingana na ripoti iliyotolewa mwezi huu ilidai kuwa wakenya hutumia hadi bilioni 766 katika michezo ya Kamari suala lililopingwa vikali na mamlaka ya kudhibiti Kamari nchini BCLB.

Mataifa mengine yanayodaiwa kuongoza kucheza Kamari ni pamoja na afrika kusini, Ghana, Uganda na Tanzania.

Subscribe to eNewsletter