Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng
MRADI huu wa kuwawezesha Wajane na akina mama wanaowalea wanao pekee yao itasaidia katika kuboresha maisha ya akina mama katika kaunti ya Marsabit.
Haya ni kwa Mujibu wa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Marsabit Naomi Jillo Waqo.
Akizungumza kwenye hafla ya kuzindua Mradi wa kuwawezeza Wajane pamoja na akina mama wanaowalea wanao pekee yao, iliyoandaliwa katika uwanja wa michezo ya Marsabit hii Leo, Naomi ameelezea kwamba kupitia afisi yake kwa ushirikiano na serekali kuu watahakikisha kuwa hakuna mjane ameachwa nyuma, kimaendeleo huku akiichangamoto washikadau kuwekeza zaidi katika kuboresha maisha ya Wajane jimboni.
Naomi ameelezea kwamba iwapo Wajane watapata mafunzo kuhusu uwekezaji na kuwezeshwa basi kutakuwa na jamii Bora ambayo itajitegemea.
Naomi amewarai akina Mama kuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha wameendeleza malezi Bora ili kukuza jamii Bora yenye maadili Mema.
Kuhusiana na suala la vitambulisho, Naomi amewataka akina Mama kuwa katika mstari wa mbele na kuhakikisha kuwa Wanao wamepata vitambulisho huku akiitaka idara ya usajili jimboni kuweza kujukumika Zaidi na kuwapa kitambulisho wanafunzi wote waliofikisha miaka 18 wakiwa shuleni.