Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Carol Waforo
Huku ulimwengu ukiendelea kuadhimisha mwezi wa uhamasishaji wa afya ya akili mwezi huu wa Mei wafanyikazi katika idara mbalimbali wametajwa kuwa kati ya watu wanaokabiliana na matatizo haya ya kiakili.
Hii ni kutokana na mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Haya yamewekwa wazi na mtaalam wa afya ya akili katika hospitali ya Rufaa ya Marsabit Victor Karani ambaye amezungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee.
Dr Karani anasema kuwa baadhi ya matatizo haya yanapelekea hata watu kijitia kitanzi huku akiwataka waathiriwa kuzungumza na kutafuta misaada kutoka kwa wataalam wa afya ya akili.
Dr Karani amewataka waathiriwa wa matatizo haya kujitokeza na kupuuzilia mbali unyanyapaa kutoka kwa jamii huku nayo jamii ikitakiwa kukomesha unyanyapaa huo.
Hapa katika kaunti ya Marsabit visa vya wafanyikazi kujitia kitanzi vimeongezeka haswa maafisa wa polisi. Siku ya Jumapili iliyopita afisa moja alijitia kitanzi katika eneo la Turbi.
Mwezi uliopita wa Aprili afisa wa polisi aliyekuwa akihudumu katika Kaunti hii ya Marsabit alifariki kwa kujitia kitanzi baada ya kuwaua watoto wake wawili na mtoto mwengine wa shemeji yake kwa kuwapa sumu katika eneo la Kakdhimu huko Rachuonyo, Kaunti ya Homa Bay.
Afisa huyo aliwacha barua alioleza masaibu aliyoyapitia kifamilia na pia kikazi.
Mwezi huu huadhimishwa ili kutilia mkazo katika umakini unaohitajika kwa umuhimu wa afya wa kiakili. Mwezi huu pia mazungumzo ya wazi yanahimizwa kwa kiasi cha juu ili kupunguza unyanyapaa unaozunguka matatizo ya afya ya akili.