County Updates, Local Bulletins

WAFANYABIASHARA WA KUSAFIRISHA SAMAKI KUTOKA ILLERET – MARSABIT WATAJA KUHANGAIKA BARABARANI BAADA YA NJIA KUSOMBWA NA LORI KUANGUKA.

Na Samuel Kosgei

Madereva na wafanyabiashara wa kusafirisha samaki kutoka barabara ya Illeret kuja Marsabit hadi Busia wametaja kuhangaika sana katika barabara hiyo baada ya mvua kusomba sehemu ya barabara na kuangusha lori lao.

Dareva wa lori la kusafirisha samaki kutoka Illeret Abdi Noor akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu kutoka eneo la Dharadhe eneobunge la North Horr ameonesha masikitiko yake akisema kuwa wanakandarasi waliopewa jukumu la kukarabati barabara hiyo ndio waliofanya kazi duni kwani kila mara kunaponyesha barabara hiyo haipitiki.

Abdinoor na wenzake ambao wamekwama baada ya lori lao kuanguka wamesema pia hali ya maisha katika eneo hilo ni ngumu ikizingatiwa kuwa hakuna mtandao wa kusaidia kuwasiliana.

Guyo Diba ambaye ni makanga wa lori hilo amearifu jangwani kuwa kwa kawaida wao husafiri kutoka eneo hilo kwa wiki moja au mbili lakini kufikia sasa wamekesha eneo hilo karibu wiki moja kuanzia siku ya jumapili.

Mohamed Doyo ambaye ni mwanabiashara anayedai kuwekeza Zaidi ya shilingi milioni moja kwa biashara hiyo ya kusafirisha samaki anasema kuwa ameenda hasara kubwa kufikia sasa kwani samaki wengi wameharibika kutokana na mvua na kunyeshea  bidhaa hiyo barabarani. Wanasema kuwa maisha yao pia yamo hatarini kutokana kukesha barabarani, kijibaridi, na hata ukosefu wa chakula.

Wametoa ombi kwa serikali ya jimbo au serikali kuu kuwasaidia kuondoka eneo hilo sawa na kukarabati barabara hiyo.

Subscribe to eNewsletter