County Updates, Local Bulletins

WACHIMBA MADINI WATAKIWA KUREJESHA MABOMU IWAPO WALISALIA NAYO, MOYALE

Na Caroline Waforo

Wachimba madini katika eneo la Heillu eneobunge la Moyale kaunti ya Marsabit wametakiwa kurejesha mabomu iwapo walisalia nayo.

Hii ni baada ya idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit kuibua hofu kuwa huenda kuna wachimba madini ambao hawakurejesha mabomu yaliyopatikana siku ya Jumamosi.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa mabomu hayo ni hatari kwa usalama sasa akitoa tahadhari kwa jamii.

Vilevile kamanda Kimaiyo amesema kuwa mabomu 23 yenye ukubwa kwa milimita 81 yaliyopatikana katika eneo hilo yaliteguliwa na Vikosi vya Ulinzi nchini KDF siku iyo hiyo ya Jumamosi.

Mabomu hayo yalifukiwa chini ya ardhi na ambayo yanaaminika kuachwa na wakoloni.

Subscribe to eNewsletter