County Updates, Local Bulletins

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA VINGALI VINAENDELEA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT ASEMA MWANAHARAKATI WA KUPAMBANA NA MIHADARATI.

Na Samuel Kosgei

Vita dhidi ya dawa za kulevya katika kaunti ya Marsabit vingali vinaendelea. Hii ni kauli yake Fredric Ochieng mwanaharakati wa kukabilianana na mihadarati katika kaunti ya Marsabit. akiongea na shajara ya radio jangwani Ochieng ameelezea hatua ambazo wamepiga kufikia sasa

Ametaja ushirikiano baina ya wakaazi na vyombo vya utawala kama kiiini cha mafanikio katika vita hivyo.

Hata hivyo Ochieng ameezea changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli ya kukabiliana na mihadarati. Ametaja kwamba kunao baadhi ya washikadau wanaolemaza vita hivyo swala linalosababisha kujivuta kwa shughuli yenyewe.

Sasa anawasihi wakaazi kushirikiana na vyombo vya utawala ili kutibua mipango ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Amesikitika kuwa huenda wanafunzi wengi wakakosa kurejea masomoni shule zinapofunguliwa kutokana na wazazi kujitosa kwa matumizi ya dawa hizo kupitia ulevi na matumizi ya mihadarati.

Subscribe to eNewsletter