County Updates, Local Bulletins

VISA VYA UNAJISI PAMOJA NA ULAWITI VIAONGEZEKA KATIKA ENEO BUNGE LA MOYALE, KAUNTI YA MARSABIT.

Na Caroline Waforo,

Visa vya unajisi pamoja na ulawiti vinaendelea kuongezeka katika eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.

Hili limebainika kutokana na ongezeko la kesi zinazohusiana na unajisi na ulawiti katika mahakama ya Moyale huku jumla ya kesi 10 zikisajiliwa katika mahakama hiyo katika kipindi cha chini ya miezi minne ya kwanza ya mwaka huu wa 2025.

Haya yamewekwa wazi na hakimu katika mahakama ya Moyale Willy Cheruiyot, ambaye amezungumza wakati wa kipindi cha Amkia Jangwani leo Jumatano.

Hakimu Cheruiyot amesema kuwa visa vya unajisi huongezeka sana msimu wa likizo ndefu, huku idadi kubwa ya visa hivyo ikikosa kuripotiwi kwa idara za usalama na kushia kusuluhushwa na wazee vijini kinyume cha sheria.

Hakimu Cheruiyot ametahadharisha jamii dhidi ya kusuluhisha visa hivyo vijijini akisema kuwa watakuchukuliwa hatua za kisheria.

Kadhalika hakimu Cheruiyot amebainisha kuwa kesi za watoto kuozwa kwa mapema pia zinashuhudiwa katika mahakama hiyo ya Moyale.

Vilevile amewataka wananchi kutambua na kujua haki zao za kisheria aidha kama mwathiriwa au mshukiwa.

Na huku mahakama ikiendelea kushabikia utumizi wa njia mbadala ya kutatua kesi nje ya mahakama maarufu kama Alternative Justice Sesytem AJS hakimu Cheruiyot amewataka wakaazi Moyale na kote jimboni Marsabit kutambua kuwa sio kesi zote zinaweza kutatuliwa kutumia mfumo huo. Kesi hizo zinajumuisha kesi za ubakaji, mauaji, wizi wa kimabavu kati ya kesi nyingine. Kesi hizi lazima zitatuliwe mahakamani.

Subscribe to eNewsletter