County Updates, Local Bulletins

VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUSULUHISHA MIGOGORO YAO KISIRI BADALA YA KUANIKA HADHARANI

Harrisson Mugo – Mwekahazina wa chama cha Nation Vision Party.

NA JB Nateleng

Viongozi wa kisiasa wametakiwa kusuluhisha migogoro yao kwa siri badala ya kuanika hadharani mabaya ya wenzao. Haya ni kwa mujibu wa mwekahazina wa chama cha kisiasa cha National Vision Party (NVP) Harrison Mugo.

Mugo ameelezea kwamba wanasiasa wanapaswa kitunziana siri badala ya kuanikana hadharani akisema hali hiyo itaadhiri umoja wa kitaifa hivyo kurejesha nchi nyuma kimaendeleo

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Mugo, amesema sio vyema kwa wanasiasa kujitokeza na kujitetea mbele ya wananchi badala ya kutekeleza ajenda ambazo ni za maendeleo.

Mugo amemtaka aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kuacha siasa ya kugawanya wananchi na badala yake aungane na viongozi wengine ili kusukuma nchi mbele.

Matamshi yake yanajiri siku moja baada ya Rais William Ruto kuweka hadharani chanzo cha Rigathi Gachagua kung`atuliwa mamlakani kama naibu wa Rais

Subscribe to eNewsletter