County Updates, Local Bulletins

VIKUNDI 40 VYA JAMII KUTOKA MAIKONA NA KARGI MARSABIT, VYAZAWADIWA SHILINGI MILIONI 12 NA SHIRIKA LISILO LA KISEREKALI LA IREMO ILI KUJIIMARISHA.

Na Isaac Waihenya,

Vikundi 40 vya maendeleo ya jamii kutoka wadi za Maikona na Kargi kaunti ya Marsabit vimenufaika na kitita cha shilingi milioni 12 kutoka kwa shirika lisilo la kiserekali la IREMO.

Vikundi hivyo vimenufaika kupitia mradi wa Survivor Commuinity Led Response (SCLR) ambao umezinduliwa hii leo na shirika la IREMO hapa mjini Marsabit.

Vikundi hivyo vinajumuisha 33 vya kijamii na 7 ambavyo ni vya wanawake wajane na watu wanaoishi na ulemavu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi wa shirika la IREMO, Lokho Abduba amesema kuwa fedha hizi zitasaidia vikundi hivyo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.

Vikundi hivyo vitanufaika na kati ya shilingi 250,000 hadi 350,000 ili kutatua baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kama jamii.

Aidha Bi Lokho ameweka wazi kuwa wanalenga wadi hizo mbili kwani ni kati za wadi zilizoadhirika wakati wa ukame uliodumu kwa takriban miaka mitatu.

Kwa upande mwasisi wa shirika la IREMO, Darare Gonche amesema kwamba mradi huo unawalenga haswa akinamama kwani wametengwa katika jamii za wafugaji.

Darare amesisitiza hoja ya jamii kuhakikisha kwamba wanaangazia mbinu mbadala ya maisha kuliko tu kutengema ufugaji pekee.

Aidha baadhi ya wanachama wa vikundi viivyonufaika wamepongeza shirika la IREMO huku wakitaja kuwa mradi huo utawasaidia kukabiliana na baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo mabadiko ya tabia nchi.

Subscribe to eNewsletter