Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Sebalua Moses
Vijana katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kupata ujuzi wa kujiajiri. Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya elimu kaunti ya Marsabit Robert Mugambi.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani Mugambi amesema kuwa vijana humu nchini wana nafasi kubwa ya kujiendeleza katika jamii na kwa hiyo ni sharti wajielimishe na hata kujitafUtia ajira ambazo zitaweza kukimu mahitaji yao kupitia mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya kiufundi. Mugambi Pia amesema kuwa Kaunti ya Marsabit ina vyuo vya kiufundi vya kutosha.
Vile vile Mugambi amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kujiunga na vyuo vya kiufundi haswa wakati huu shule zinapofunguliwa. Aidha amesema kuwa ni sharti vijana waweze kujitaftia ajira kupitia kwa mafunzo wanazopata katika vyuo vya kiufundi huku akiwahimiza kutokaa manyumbani kungoja nafasi za kazi kutokea .
Wakati huo huo Mugambi amesema kaunti ya Marsabit imeweka mikakati ya kutosha na kuboresha elimu ya vyuo vya ufundi akiwahimiza vijana kuwa watapokea mafunzo hayo bila malipo