County Updates, Local Bulletins

VIJANA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA WATISHIA MAISHA WAZAZI WAO, MOYALE.

Picha Hisani

Na Caroline Waforo,

Vijana amabo ni waraibu wa dawa za kulevya wanawatishia maisha wazazi wao ili kuwapa fedha za kununua dawa hizo katika eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.

Haya ni kulingana na Willy Cheruiyot ambaye ni hakimu katika mahakama ya Moyale kaunti ya Marsabit.

Hakimu Cheruiyot akizungumza na Radio Jangwani wakati wa kipindi cha Amkia Jangwani leo Jumatano amesema kuwa visa hivyo vya vijana kutishia kuwaua wazazi wao vimeongezeka kwa kiwango kikubwa katika eneo bunge hilo na kusababisha ongezeko la kesi nyingi za kutishia kuua katika Mahakama ya Moyale.

Kesi pia za kuumiza watu zimesajaliwa katika mahakama hiyo ya Moyale huku hakimu Cheruiyot akisema kuwa nyingi ni miongoni mwa vijana.

Haya yanajiri huku utumizi wa dawa za kulevya ukiwa donda sugu katika kaunti ya Marsabit na haswa eneo bunge la Moyale na kutajwa kuchangiwa pakubwa na mpaka wa Kenya na Ethiopia ambao unatumika katika ulanguzi wa mihadarati na dawa za kulevya.

Subscribe to eNewsletter