Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
NA JB Nateleng
Vijana wa kanisa Katoliki kutoka eneo la Sagante (Sagante Zone) parokia ya Cathedrali hapa Jimboni Marsabit wameandaa warsha ya pamoja kwa ajili ya kujua na kufahamu kuhusu neno la Mungu.
Hafla hii ambayo iliwaleta pamoja vijana kutoka kigango cha Manyatta Jillo, Athi Huka, Goro Rukesa Dub Gobba pamoja na Gar Qasa imedhamiria kuwaelimisha vijana kuhusu Biblia, na jukumu la vijana katika kanisa.
Padri Abraham Ali ambaye ni mmoja wa viongozi wa kanisa kwenye hafla hiyo amewachangamoto vijana hawa kuweza kuwa na uelewa wa neno la Mungu ili kujenga jumuiya dhabiti ambayo itasaidia katika kuimarisha imani yao kwa manufaa ya kujenga kanisa imara.
Aidha Padre Abraham amewataka wazazi pamoja na viongozi wa kanisa kuwa karibu na vijana na kuwafunza maana ya kusali na kudumu katika sala
Kauli yake Padre Abraham imeungwa mkono na mwenyekiti wa vijana katika eneo la Sagante Gabriel Galgallo Boru ambaye amesema kuwa vijana katika eneo hilo wamekumbwa na changamoto si haba ambayo yanafaa kuangaziwa kwa kina