Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai,
Matumizi mabaya ya mitandao,utumiaji wa dawa za kulevya na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa maswala yanayoajiri umoja wa jamii.
Hayo yamewekwa wazi katika kongamano la kila mwaka la vijana wa kanisa la kiangilikana hapa jimboni Marsabit.
Akiongea na idhaa hii Askofu wa wa kanisa la kiangilikana daosisi ya Marsabit, Askofu Qampicha Wario amewarai viongozi katika nyanja mbalimbali kuwadhamini vijana kwa manufaa ya nchi.
Aidha Askofu Qampicha amewataka wananchi na viongozi kudumisha heshima baina yao kwani mienendo yao inategemewa sana katika mustakabali wa jamii.
Kauli hii imeungwa mkono na mchugaji Canon Kargi Denge ambaye ameelezea kuwa ujuzi wa vijana katika maswala ya tekolojia unachangia pakubwa katika kuhatarisha maisha ya vijana haswa iwapo hautatumika ipasavyo.